TECHNOLOGIA YA COMPUTER
TECHNOLOGIA YA COMPUTER
COMPUTER SERVICES
Karibu tena mtanzania mwenzangu katika tovuti hii mpya ,Utapata habari nyingi zinazo husiana naTechnologia ya sasa.Mimi kama mtanzania mwenzako nimechukua fursa hii kuamasisha watanzania wa leo kutumia zaidi Technologia ya kileo ili kutimiza ndoto zao ,Je Ni vitu gani kuwa navo ili kutimiza ndoto zetu. Pia Kutakuwa na Makala zinazo elezea matumizi mazuri ya computer ,kuteneza home network, bila ya kutumia vifaa vingi na vya gharama,je ni computer gani inafaa kwa matumizi yako,na ipi haifai kwa matumizi yako.Karibu sana wapenzi wasomaji .
SOMA MAKALA MBALIMBALI ZINAZO HUSIANA NA TECHNOLOGIA YA SASA
Moja ya Makala muhimu na watu wengi wanapenda Zaidi ni hasa kujua maisha ya mafanikio yanapatika vipi , je wewe mtanzania wa leo unaitaji kukua kiuchumi . Basi Usikose mada hizi tutakazo kuwa naza katika blog yetu hii Nzuri
kwa leo Nitapenda kukupa Ufahamu Kidogo Kuhusiana na Computer ,
JE COMPUETER NI NINI?


Vile vile Computer tutaweza kusema ni kifaa kinacho weza kukurahisishia wewe mtanzania kuingia internet na kufanya shughuli zako mtandaoni mfano mzuri unapo tuma email, unapo chati katika mitandao ya kijamii kama facebook,twiter,nk tutajifunza mengi kuhusu internet endelea kusoma mada hii ili kujua mengi Zaidi ,
Wavuti ni nini, na ni jinsi gani unavyoweza kuifanyia kazi?
Unavyochunguza vidokezo juu ya usalama katika Vizuri Kufahamu, unaweza ukawa na maswali kadhaa kuhusu wavuti ni nini na jinsi ya kutumia aina maarufu ya huduma mtandaoni. Tafadhali angalia majibu haya kutoka Googlers na pata maelezo zaidi kuhusu kuingia mtandaoni, kupata maelezo na kuabiri katika mtandao, na kuunganisha na kushiriki mtandaoni.
Intaneti ni mtandao wa kompyuta zilizoenea duniani kote zote zikiwa zimeunganishwa moja kwa nyingine. Unapojiunga kwenye Intaneti unakuwa na ufikiaji wa World Wide Web, ambayo ni sawa na maktaba iliyojaa kurasa za maelezo.
Unaunganishwa vipi kwenye Intaneti? Shughuli ya ISP ni ipi?
Kabla hujaanza kuuchunguza mtandao, utahitaji kuweka mpango na ISP. ISP, au Mtoa Huduma za Intaneti, ni kampuni inayokuruhusu kufikia Intaneti na huduma nyingine za mtandao. Wanatoa njia tofauti za kuunganishwa ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kebo, fiber optics au Wi-Fi. Muunganisho hizi tofauti huamua kasi ya ufikiaji wako wa mtandao.

Computer ina matumizi mengi sana ukiwa nyumbani,kwako mwanafunzi, pia hata maofisini ,pia unaweza ukajiajili kupitia computer yako hapo ulipo
Kwa mwanafunzi utaweza kusomea computer pamoja na kutafuta mengi kwenye internet, kwa mfanya biashara utatunza kumbukumbu zako za kibiasha pia hata za kiofisi
Unaweza kutengeneza pesa kupitia computer yako ya nyumbani kama utakuwa mbunifu wa kujitangaza kupitia computer yako.Blogger ni njia pekee inayo weza kuitangaza biashara yako kwa kasi na kwa watu wengi duniani ,Blog ni mfano wa website ambayo unaweza kuweka matangazo yako ya kibiashara pamoja na kujitangaza wewe ni nani ?
Ni rahisi sana kutengeneza blog yako na kujitangaza Zaidi, pia nitakuelekeza jinsi ya kuanzisha blog yako ya kibiashara pamoja na kupata muonekano mzuri zidi wa blog yako
Mara nyingi unapo tengeneza blog itakulazimu uwe katika internet lakini kuna njia mbali mbali za kutengeneza blog kuonekana katika muonekano mzuri Zaidi kwa kutumia Microsoft word, Microsoft publisher pamoja na Excell, Sio hivo kuna lugha mbali mbali za kutengeneza kurasa za blog yako
Kuna mfano wa lugha ina itwa HTML, CSS, JavaScript ni lugha nzuri za kutengeza kurasa zako za blog yako yote hayo utayapata hapa katika tovuti yetu hii ya hlmservice.
COMPUTER GANI INA FAA KWA MATUMIZI YAKO

Unaweza ukawa na home network nzuri inayo weza kukidhi mahitaji yako kabisa kwa kutumia simu yako ya smart phone, Hapa inakuwa haina haja ya kutumia modem kutengeneza network nyumbani hata oficine ,Kupitia simu yako ya smartphone unaweza kutengeneza wireless inayo weza kumudu kwa computer Zaidi ya tatu hadi nne kikubwa ni kujiunga vifurushi vya internet kama kawaida ya vifurushi vya mitandao yote alafu tengeneza wireless yako ufurahie internet na yenye kasi Zaidi
Jinsi ya kutengeneza wireless kwa kutumia smartphone yako fuata hatua zifuatazo
Hatua ya kwanza
Ingia Katika sehemu ya setting kwenye simu bofya Mahali pameandikwa More..Utaona maelezo haya juu kabisa pameandikwa Wireless&Networks chini yake utaona
Airplane Mode
Vpn Settings
Tethering & Portable hotspot
Mobile Networks
Hatua ya pili
Bofya mahali wameandika Tathering & Portable hotspotitakuonesha jinsi ya kuiwasha wireless yako lakini kabla ya yote unahitaji kuitengeneza kwa jina unalo taka kwa kubofya mahali pameandikwa Set-up Wi-Fi hotspot ,Andika jina upendalo pia kuna mahali pa kuweka passwork kama unahitaji kwa jili ya kuzuia watu wengi kutumia wireless yako basi andika passwork na iwe siri kwako tu ,Endapo utasambaza password yako utaona matumizi yako ya bundle ni makubwa kwa sababu utakuwa umeruhusu watu wengi watumie wireless yako
Hizo hatua mbili juu ni kwa wale watu wanao tumia simu za Android lakini kwa wanao tumia windows phone ni rahisi Zaidi kwani utaenda mahali pameandikwa setting halafu Internet sharing,Uta seti password na jina la wireless yako.
Kabla ya kufanya yote hayo hakikisha computer yako ina support wireless kama hapana basi angali kama kuna driver za wireless kama computer itakuwa hai support basi zoezi hili litakuwa gumu kwako.
Comments
Post a Comment